Ofa inaisha baada ya masaa 48, au nafasi 50 zikiisha.
⏰ Umebakia muda huu ofa hii kuisha
48
00
00
Kwa wafanyabiashara na network marketers wanaouza kupitia WhatsApp
“Nililipia Matangazo. Inbox Ikajaa Wateja. Lakini Bado Nilikuwa Nakesha Usiku Nikisave Namba Moja Moja Kuongeza Status Viewers… Mpaka Siku Nilipojiuliza Swali Moja Lililobadilisha Kila Kitu.”
Jinsi nilivyoacha kukesha, nikaanza kuonekana kwa wateja wangu kila siku na kuongeza trust, na mauzo yangu yakaongezeka. Na jinsi wewe unavyoweza kujaribu kitu hicho hicho BURE, leo.
✅ Jaribu kwanza, ulipe baadaye. 🛡️ Guarantee ya siku 14 ya kurudishiwa pesa yako yote.
Mpendwa Mfanya Biashara!…
Nataka nikwambie kitu ambacho hujawahi kuambiwa waziwazi.
Kuna kipindi nilikuwa kwenye network marketing.
Nilikuwa na bidhaa nzuri. Nilikuwa na ndoto kubwa. Na nilikuwa tayari kutumia pesa yangu mwenyewe kwenye matangazo ya kulipia.
Na matangazo yalifanya kazi vizuri sana.
Simu yangu ilikuwa inalia kila dakika. WhatsApp Notifications…
Bei gani?Inapatikana wapi?Naomba maelezo.
Inbox ilijaa watu.
Lakini hapa ndipo nilipoanza kuumia…
Wateja walikuwa wanakuja wengi, lakini nilikua nashindwa kuuza.
Mtu anauliza bei leo, kesho mazungumzo yake yameshuka chini ya chat nyingine 200.
Wiki ijayo hata simkumbuki. Na yeye hanikumbuki mimi.
Nilikuwa nalipia kuwaleta watu… halafu nawapoteza kwa mikono yangu mwenyewe.
Nikajifunza kitu kimoja ambacho ndio kilibadilisha kila kitu: kua inatakiwa nijenge trust, watu waniamini kabla sijawauzia. Na ndipo ilibidi lazima wanione kila siku kwenye status, hata kama hawajanunua.
Narudi kwenye group. Namba nyingine. Nasave. Tena. Na tena.
🕛 Saa sita usiku. 🕐 Saa saba.
Macho yanauma. Kidole kinauma. Na bado group lina mamia ya namba ambazo sijazigusa.
Asubuhi naamka nimechoka… lakini bado nadaiwa kitu kimoja: kupost status.
Ili kujenga trust, wanijue na waniamini kabla hawajanunua.
Na hapa nitakuwa mkweli kwako.
Kuna siku sikupost kabisa. Sikuwa na mood. Nilikuwa nimechoka tu.
Kuna siku nilikuwa ndani ya daladala kuelekea kazini. Najua nahitaji kupost, lakini nimebanwa, simu iko mkononi, na kichwani hakuna hata caption moja nzuri inayokuja.
Na kila siku nisiyopost, nilijua ukweli mmoja unaouma:
Wateja wangu wanamwona mshindani wangu, na si mimi.
Status zangu ziliongezeka, ndiyo. Lakini kwa shida sana. Ilikuwa kama kujaza maji kwenye ndoo yenye tundu.
Swali lililobadilisha kila kitu
Siku moja nilikaa nikajiuliza:
“Kwa nini nafanya kwa mikono kazi ambayo AI inaweza kuifanya kwa sekunde tu?”
Hapo ndipo nilipogundua jambo ambalo wauzaji wengi hawalioni.
Tatizo langu halikuwa kupata watu. Watu nilikuwa nawapata wengi.
Lakini…
Tatizo lilikuwa kuendelea kuwafikia. Siku baada ya siku. Mpaka waniamini. Mpaka wanunue.
Basi hapo ndio safari yangu ilipoanza. Nilijifunza kutoka kwa watu tofauti tofauti na kununua kozi mbalimbali kutoka kwa wataalamu hapa Tanzania, Kenya, Nigeria na India.
Na hapo ndipo nikapata wazo la kutengeneza hii mifumo miwili.Mwanzoni, kwa ajili yangu mwenyewe tu.
📇 Mfumo wa kwanza
Smart Contacts Autosave
Napiga screenshot namba zote za group, kisha naipakia kwenye mfumo huu. Na ndani ya sekunde chache, majina na namba zinakua saved automatic, zinaingia kwenye Google Contacts zangu.
Kazi iliyokuwa inanikesha usiku mzima… sasa inachukua dakika chache tu.
🎬 Demo: Smart Contacts Autosave
📅 Mfumo wa pili
Status Auto Post
Siku moja nikiwa na utulivu na mood nzuri, naandaa status zangu zote za wiki nzima au mwezi: picha, video, maandishi, hata sauti. Na captions nilizoziandika kwa akili iliyotulia.
Halafu mfumo unazipost kwa wakati wake automatically, wiki au mwezi mzima, bila kushika simu kupost status.
Hata niwe ndani ya daladala. Hata niwe nimechoka. Hata nisiwe na mood.
Wateja wangu wananiona kila siku na wanazidi kujenga trust bila kutumia nguvu.
🎬 Demo: Status Auto Post
Na unajua nini kilitokea?
Watu walianza kuniona kila siku, consistently. Wakaanza kuniamini.
Follow-up ikawa rahisi, kwa sababu namba ziko kwenye simu na mimi niko kwenye status kila siku.
Mtu aliyeuliza bei wiki tatu zilizopita anarudi mwenyewe baada ya kuniona mara kwa mara kwenye status:
Ile bidhaa bado ipo?
Mauzo yangu yakaongezeka. Na kwa mara ya kwanza… nililala usiku nikiwa nimetulia. 😌
Sasa, nikuulize maswali manne
Ni namba ngapi ziko kwenye magroup yako au inbox sasa hivi, tangu mwaka ulioanza biashara, hujazisave?
Ni siku ngapi mwezi huu hukupost status?
Ni wateja wangapi walikuulizia bei… halafu wakapotea?
Umepoteza namba ngapi tokea umeanza biashara hiyo? Vipi kama ungekua umezisave zote?
Barua hii ni kwa ajili yako kama…
Uko kwenye network marketing au unafanya mauzo kwa biashara yoyote kupitia WhatsApp
Unalipia matangazo, watu wanakuja inbox, lakini wengi wanapotea
Uko kwenye magroup yenye mamia ya namba ambazo hujazisave
Umewahi kukesha ukisave namba moja moja
Kuna siku hupost status kwa sababu umechoka, uko bize, au huna mood
Kama umejiona hata kwenye mstari mmoja katika barua hii, basi… endelea kusoma. 👇
Nimerekodi video fupi ili uone kwa macho yako jinsi mifumo yote miwili inavyofanya kazi:
🎬 Demo: Jinsi mifumo yote miwili inavyofanya kazi
Sasa Nina Ofa Maalumu Kwa Ajili Yako
Kama umechoka kuhifadhi namba za wateja mmoja mmoja, au unashindwa kupost status kwa sababu ya majukumu mengi… sikiliza hili kwa makini.
Bei ya kawaida ya kila mfumo ni TSh 25,000 kwa mwezi.
Lakini kwa saa 48 tu, mambo ni tofauti kabisa.
Hatua ya 1 Chagua mfumo mmoja wa kulipia
Chagua ule unaokuumiza zaidi leo:
📇 Smart Contacts Autosave
Save namba automatically. Mamia ya namba zinaingia kwenye Google Contacts zako ndani ya sekunde chache. Hutakesha tena.
Panga status za wiki au mwezi mzima mara moja: picha, video, maandishi, hata sauti. Zinatoka kwa wakati uliopanga wewe, hata ukiwa bize au uko barabarani.
Hulipi hata shilingi moja leo. Jaribu kwanza BURE.
Usiporidhika ndani ya siku 14, unarudishiwa pesa yako yote.
🔒 Na bei yako inafungwa milele
Bei itarudi TSh 25,000 kwa mwezi kwa wateja wapya.
Wewe ukiingia leo, utaendelea kulipa TSh 10,000 kwa mwezi, muda wote utakaoendelea na subscription. Mwaka huu. Mwaka ujao. Hata miaka mitatu ijayo.
Bei ikipanda kwa wengine… wewe hutaguswa.
🛡️ Guarantee ya 100%: Risk yote iko kwangu
Nataka uwe na uhakika kamili. Kwa hiyo nimekuwekea kinga mara mbili:
✅ Kinga ya 1: Jaribu kwanza, ulipe baadaye.
Hulipi hata shilingi moja leo. Kwanza unajaribu mfumo BURE na kuuona kwa macho yako ukifanya kazi kwenye simu yako. Ukiridhika, ndipo unalipia.
✅ Kinga ya 2: Siku 14 za kurudishiwa pesa yako yote.
Ukishalipa, na ndani ya siku 14 ukaona mfumo haukufai, kwa sababu yoyote ile, niambie tu. Nitakurudishia TSh 10,000 yako yote. 100%. Hakuna maswali. Hakuna kubishana. Hakuna kuzungushwa.
Huna cha kupoteza. Risk yote nimeibeba mimi.
Kwa nini ufanye uamuzi sasa
Sababu ni mbili. Na zote ni za kweli:
1
Ofa inafungwa baada ya masaa 48, au nafasi 50 zikiisha.
Baada ya hapo, bei ya TSh 10,000 iliyofungwa milele na zawadi zote mbili hazitapatikana tena.
2
Nafasi ni 50 tu.
Nakusetupia kila mteja mimi mwenyewe. Siwezi kuwahudumia vizuri watu wengi zaidi ya hao kwa awamu hii. Nafasi zikijaa kabla ya muda kuisha, ofa inafungwa mapema.
Unachotakiwa kufanya sasa hivi ni rahisi
1
Bonyeza kitufe hapa chini.
2
WhatsApp itafunguka na ujumbe uko tayari. Tuma tu.
3
Nakufanyia setup, unajaribu BURE, na unaona mwenyewe.
Je, bado unafikiria? Endelea kusoma maswali hapa chini 👇
Nilitengeneza mifumo hii kwa sababu ningetamani ningekuwa nayo siku ile nilipokuwa nakesha nikisave namba. Sitaki upitie nilichopitia.
Ni mimi Ninaejali Biashara Yako,
Kinganije Juma
Halal Business
P.S. Kumbuka unachopata leo: mfumo mmoja kwa TSh 10,000 tu kwa mwezi, mfumo wa pili BURE kwa mwezi mzima, setup ya bure, na guarantee ya 100% ya kurudishiwa pesa. Kitu pekee unachoweza kupoteza ni nafasi hii, kwa sababu inafungwa baada ya saa 48.
P.P.S. Kama unalipia matangazo, kumbuka: kila mtu anayeingia inbox kwako, umemlipia. Usiendelee kuwapoteza.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
❓ Namba zangu ziko salama?
Ndiyo. Namba zinahifadhiwa kwenye Google Contacts ya akaunti yako mwenyewe, si kwangu. Na app imepitia ukaguzi wa usalama wa Google (Google OAuth verification).
❓ WhatsApp yangu inaweza kufungiwa (ban)?
Smart Contacts Autosave haigusi WhatsApp kabisa. Inasoma screenshot ulizopiga kwenye simu yako tu, na kusave namba kwenye Google Contacts.
❓ Inafanya kazi kwenye simu yangu?
Mifumo hii imetengenezwa kwa simu za Android. Kwa iPhone, ni Smart Contacts Autosave tu. Tutafanya demo na kuangalia kama simu yako inafaa kabla hujalipia chochote.
❓ Mimi si mtaalamu wa teknolojia. Nitaweza?
Ndiyo. Ndiyo maana nitakufanyia setup mwenyewe, bure. Ukijua kupiga screenshot, unajua kutumia mfumo huu.
❓ Nalipa mara moja au kila mwezi?
Kila mwezi. Kupitia ofa hii unalipa TSh 10,000 kwa mwezi kwa mfumo uliouchagua, na bei hiyo inabaki hivyo hata bei ya kawaida ikipanda.
❓ Nikibadilisha simu, namba zitapotea?
Hapana. Ziko kwenye Google Contacts. Ukiingia na akaunti ile ile ya Google kwenye simu mpya, zinarudi zote.
❓ Nikiacha kulipia, nini kinatokea?
Mfumo unasimama. Lakini namba zote ulizosave zinabaki zako milele kwenye Google Contacts. Ila ukiacha, unapoteza bei ya ofa ya TSh 10,000 iliyotolewa.
❓ Kwa nini bei iko chini hivi? Kuna ujanja?
Hakuna ujanja. Nataka wateja wa kwanza watakaotumia mifumo hii, kunipa maoni yao na ushuhuda wa uzoefu wao. Wewe unapata bei ya chini milele, mimi napata watu wanaoniamini. Sote tunashinda.
Bado una swali ambalo halijajibiwa? Niulize moja kwa moja 👇